Wednesday, 28 May 2014

Mastaa hawa wajiweka kitanzini baada ya video ikionyesha wanavuta bangi kuvuja






Mastaa hawa wajiweka kitanzini baada ya video ikionyesha wanavuta bangi kuvuja.


one


Wakati wakiwa kwenye ziara yao nchini Peru, Nyota wa kundi la One
Direction Zayn Malik na Louis Tomlinson wameonekana wakivuta bangi
wakiwa njiani na tukio hilo kuvuja kwa njia ya video hali iliyopeleka
baadhi ya mashabiki wa shoo yao kuchoma moto tiketi za ziara hiyo.


one2
Chombo kimoja cha habari kimefanikiwa kuidaka video hiyo ya dakika 5
ikionyesha nyota hao wakivuta bangi na kuongea maneno yaliyowakera
baadhi ya mashabiki wao.


one3
Baadhi ya mashabiki walikasirishwa sana na kipande cha video hiyo na
kuwazungumzia mastaa hao kuwa hawajali mashabiki wao ambao wengi ni
vijana na kuwafundisha tabia zisizofaa huku wengine wakiweka picha
mitandaoni wakiwa wanachoma tiketi za shoo hiyo.


Ungependa stori kama hizi zisikupite? niko tayari kukutumia wakati wowote mtu wangu, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.

No comments:

Post a Comment