Majeruhi
wa pili mke Chacha Wambura bi Happiness Chacha (22) akiwa amelazwa
katika wodi namba 8 katika hospitali ya wilaya ya Geita baada ya kuungua
moto yeye na mme wake-Picha zote na Valence Robert
|
Wanandoa
wawili wakazi wa kijiji cha Lwamgasa wilayani
Geita mkoani Geita Happiness Chacha(22)
na mme wake Chacha wambura(35) wamenusurika kufa baada ya nyumba yao kuungua
moto katika kibanda chao cha bar.
Tukio
hilo limetokea jana usiku saa nane usiku katika kijiji cha Lwamgasa ambapo
kufuatia tukio hilo majeruhi wakikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Geita
mkoani Geita walipolazwa wodi namba 7 na 8.
Robina Isack anayewauguza amesema kuwa usiku huo
wa saa 8 waliona moto unawaka bila kujua umeanzia wapi huku wakishangaa kwa
vile hawatumii nishati hiyo ya umeme na wala hapakuwa na moto waliokuwa
wamewasha ndani.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
|
No comments:
Post a Comment