MAREKANI YAIKABIDHI JESHI LA MAJI, MTAMBO WA MAWASILIANO WA MASAFA MAREFU
Balozi
wa Marekani Nchini Lt.Kevin Balisky akisoma risala mbele ya mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima wakati wa halfa ya
kukabidhi mtambo
wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa jeshi la maji, masaada huo
umetolewa na Serikali ya Marekani kupitia mradi wa AFRICO,leo jijini
Dar es salaam.
Naibu Waziri
wa Mambo ya ndani Pereira Silima, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
halfa ya kukabidhi mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa
kikosi cha askari wa maji akitoa shukrani kwa Balozi wa Marekani nchini,
Lt. Kevin Balisky wa pili kushoto leo jijini Dar es Salaam, ,
anayesikiliza ni bw. Norman wa Ubalozi wa Marekani,
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani, Pereira Silima (kulia) akizindua mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa kikosi cha askari wa maji katika halfa iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Balozi wa Marekani nchini, Lt. Kevin Balisky,mtambo huo umetolewa na Serikali ya Marekani
kupitia mradi wa AFRICO kwa ajili ya kusaidia kudhibiti uhalifu wa
majini na kuweza kutambua vyombo na shughuli zote zitakazofanyika katika
maji.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Pereira(kulia) Silima akisiliza maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa mawasiliano Norman(katikati) kuhusu utendaji kazi wa mtambo wa mfumo
wa mawasiliano wa masafa marefu kwa ajili ya kudhibiti usalama wa
majini kwa kikosi cha askari maji leo jijini Dar es Salaam, anayeangalia
kushoto ni Balozi wa Marekani nchini, Lt. Kevin Balisky.
Naibu
Waziri wa Mambo ya ndani Pereira Silima, (wa nne kulia) akiwa katika
picha ya pamoja ya viongozi wa jeshi la Polisi na Balozi wa Marekani
nchini Lt. Kevin Balisky (wa tatu kulia waliokaa) katika halfa ya
kupokea msaada wa mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa
kikosi cha askari wa maji katika halfa iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kikundi
cha Burudani kikitumbuiza katika hafla ya kukabidhi mtambo wa mfumo wa
mawasiliano wa masafa marefu kwa ajili ya kudhibiti usalama wa majini
kwa kikosi cha askari maji leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Lorietha Laurence-Maelezo
No comments:
Post a Comment