Leo ni Kumbukumbu ya mwaka 1 toka Albert Mangwea afariki.
ni mchana May 28 2013 ndipo zilipotoka taarifa ambazo kulingana na
ukubwa wa jina la mangwea Tanzania hakuna aliyekua tayari kuamini kama
ni kweli Mangwea kafariki dunia,zilianza taratibu za kuthibitisha
taarifa hizi ambapo baadae ilithibitika kweli Mangwea amefariki dunia.
sasa ripoti kutoka hospitali ya South Africa familia haijawa tayari
kuiweka wazi,kutoka Morogoro nimepata taarifa kuwa leo kutakuwa na ibada
asubuhi kisha jioni kutakua na tamasha la kumkumbuka Mangwea ambapo
itakua ni kumchangia mama yake Mangwea na imeandaliwa na baadhi ya wadau
wa Morogoro na kupata baraka toka kwa Familia ya Mangwea.
No comments:
Post a Comment