KUMBUKUMBU YA MANGWEA WASANII KIBAO WAFURIKA KWENYE IBADA.
Padri Octaviani Msimbe akiongoza ibada ya kumbukumbi ya kifo cha Albart Mangweha nyumbani kwao Kihonda 'Mazimbu Road' Morogoro
Padri Msimbe
Padri Msimbe akisalimiana na mama mzazi wa Mangweha Bi Denisia Mangweha
Mama Mangweha akipokea sakrameti takatifu
Mchumba wa Mangweha Michelle Louise raia ya Uingereza akihojiwa na Mtandao huu muda mfupi uliopita
Msanii wa
bongofleva Mgaza Pembe' M-2 THE- P ambaye alikuwa na m,arehemu Mangweha
Afrika Kusini akipiga picha matukio ya lbada hiyo,
Mama Mangwea akitoa shukrani kwa watu walioshiriki lbada hiyo.
Na Dustan Shekidele, Morogoro.
FAMILIA ya msanii nyota wa muziki wa Bongofleva marehemu Albert Keneth
Mangweha aliyefariki ghafla nchini Afrika Kusini May 28 mwaka jana, leo
may 28 familia hiyo imefanya ibada nje ya viwanja vya nyumba yao
iliyopo Kihonda 'Mazimbu Road' mkoani Morogoro,ya kumbukumbu ya mwaka
mmoja wa kifo cha mpendwa wao huyo aliyekuwa na nyota ya kupendwa na
wengi.
Katika lbada hiyo iliyoongozwa na Paroko wa katika la Mtakatifu Monica
Kihonda Padria Octaviani Msimbe ilihudhuliwa na wasanii kipa pamoja na
mchumba wa marehmu Mangweha Michelle Louise.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo mama mzazi wa msanii huyo
Bi,Denisia Mangweha, baada ya kukamilika kwa lbada hiyo leo jioni katika
ukumbi wa Samaki Samaki Kihonda kutafanyia shughuri nyingine ya
kumkumbuka msanii huyo.
" Pale Samaki samaki kutakuwa na shughuri mbili ya kwanza itaanza saa 12
jioni hadi saa mbili usiku na mafariki wa marehemu watafanya shughuri
yao kuanza saa 2 usiku hadi majogoo hivyo tunawakaribisha wote mliofika
kwenye ibada hii na mungu awabariki kwa kunikimbilia toka kifo cha
mwanangu,mapaka hii leo sina cha kuwalipa mungu atawalipa asanteni
sana"alisema mama huyo mwenye uso wa upole.
No comments:
Post a Comment