KIFO CHA RACHEL HAULE:utabili wa kumbiana kwa recho ni uzuni tupu,odama abaki na siri nzito,soma zaidi hapa saa 23 alizopigania uhai wake kabla hajafariki !!
KUJIFUNGUA
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichokuwepo kwenye Hospitali ya Lugalo, Recho alikuwa akisumbuliwa na tatizo la presha ya kupanda, kisukari na kifafa cha mimba.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichokuwepo kwenye Hospitali ya Lugalo, Recho alikuwa akisumbuliwa na tatizo la presha ya kupanda, kisukari na kifafa cha mimba.
Chanzo
hicho kilieleza kuwa, kwa zaidi ya saa 23 tangu afikishwe hospitalini
hapo, Recho aliteseka kwani madaktari walikuwa wakihangaika kuishusha
presha ili kuweza kunusuru uhai wake hivyo staa huyo alipigania uhai
wake kwa masikitiko makubwa.
“Tulipomfikisha
alifanyiwa vipimo, ikagundulika ana tatizo la presha na kisukari na
hata alipojifungua alipata kifafa cha mimba ndipo hali ilipozidi kuwa
mbaya,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina.
UTABIRI WA KUAMBIANA
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, pamoja na jitihada za madaktari kuhakikisha wanaokoa maisha ya mwigizaji huyo na mwanaye, walifanikiwa kumfanyia oparesheni, mtoto wa kiume akatoka salama lakini muda mchache baadaye alifariki dunia huku Recho akiwa katika hali mbaya.

siku
chache zilizopita tulitoa habari iliyomhusu Recho juu ya marehemu
Kuambiana aliyemtabiria kuwa atajifungua mtoto wa kiume iliyokuwa na
kichwa cha habari kilichosomeka: “Kuambiana alimtabiria mtoto Recho”.
Katika
habari hiyo, Recho alieleza namna alivyokutana na Kuambiana na
kumtabiria kuwa atajifungua mtoto wa kikume, kweli ikatimia kwani
alijifungua mtoto huyo lakini bahati mbaya alifariki dunia hivyo kuacha
huzuni kubwa.
Utabiri
huo ulipotimia Jumapili iliyopita, uliibua simanzi nzito kwa baadhi ya
wasanii hasa baada ya mtoto kufariki dunia huku wengi wao wakikumbuka
utabiri alioutoa Kuambiana.
KUHAMISHIWA MUHIMBILI
Baada ya madaktari wa Lugalo kuona tatizo linazidi, Jumatatu iliyopita walilazimika kumhamisha Recho katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Baada ya madaktari wa Lugalo kuona tatizo linazidi, Jumatatu iliyopita walilazimika kumhamisha Recho katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
“Ilibidi
apewe ‘transfer’ ya kwenda Muhimbili kwani hali yake haikuwa nzuri hasa
baada ya kujifungua na kupata kifafa cha mimba, akalazwa ICU,” kilisema
chanzo hicho.
MADAKTARI WAMFICHA MCHUMBA’KE
Taarifa kutoka Muhimbili zilidai kwamba baada ya kuona umati wa wasanii wa Bongo Movies usiku hospitalini hapo, madaktari walilazimika kumficha mchumba wake, George Saguda pamoja na wasanii wengine kwani walitambua pigo walilolipata hivi karibuni kwa kuondokewa na mwigizaji Kuambiana.

“Waliona
watawaongezea majonzi kwa kuwapa taarifa za msiba hivyo wakalazimika
kuwaficha hadi Jumanne asubuhi ndipo wakatoa taarifa za kifo,” alisema
nesi mmoja wa Muhimbili bila kutaja jina.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Recho na shosti yake kipenzi, Jennifer Kyaka ‘Odama’ wawili hao walikuwa watu wa karibu mno.
Ilielezwa kwamba Recho na Odama walikuwa wakishirikiana kwa kila jambo hivyo atakuwa amebaki na siri nzito Recho.
“Marehemu
amemuachia siri nzito sana Odama, walikuwa wakishirikiana katika kila
kitu na kutunziana siri nyingi nje ya kazi ya sanaa,” kilisema chanzo
hicho.
Recho
alilelewa na bibi yake baada ya kufiwa na wazazi wake wote hivyo
mipango ya kumsafirisha marehemu iliendelea kufanyika juzi Jumanne
ambapo wasanii walitarajia kuchangisha shilingi milioni kumi kufanikisha
shughuli ya kuaga, majeneza (mama na mtoto) na kusafarisha msiba kwenda
nyumbani kwao Songea, leo Alhamisi.
Mpaka
Recho anapatwa na umauti, alikuwa akijulikana zaidi kwa jina la Rachel
Haule lakini kwa mujibu wa mama yake mdogo ambaye jina halikupatikana,
marehemu alibatizwa kwa jina la Sheila Haule.
Recho
aliyezaliwa 1988, aliingia kwenye fani ya uigizaji mwaka 2009. Baadhi
ya filamu alizocheza ni pamoja na Loreen, Unpredictable, Danger Zone,
Men’s Day Out, Vanessa (yak wake mwenyewe na nyingine. Fuata makala
ukurasa wa 9. Sisi wote tu mavumbi, mavumbini tutarejea. Mungu ailaze
roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
No comments:
Post a Comment