HOFU YATANDA WASAMARIA WEMA WAINGIA MITINI DHAMANA YA WAZAZI WA MTOTO WA BOKSI
Watuhumiwa
waliofikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi ni Rashid
Mvungi (47), mama mlezi, Mariam Said (38) na mume wake Mtonga Omar
(30).
Washitakiwa
hao walifikishwa katika mahakama hiyo chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Mary Moyo, Jumatatu ya wiki hii na kusomewa mashitaka hayo huku muda
mwingi wakionesha kujutia kosa hilo ambalo hawakujua kama ni bomu ambalo
litakuja kulipuka.
Muda
mwingi, Mvungi akiwa mahakamani hapo alikuwa akiweka mikono juu ya
kichwa (angalia picha) jambo lililotafsiriwa kwamba ni kuonesha kujutia
tukio hilo.
Wakili
wa Serikali, Sunday Hyera alisema washitakiwa walitenda kosa hilo kati
ya Desemba, mwaka 2010 na Mei, mwaka huu katika Mtaa wa Azimio Kata ya
Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro.
Wakili
huyo alidai kuwa katika kipindi hicho, washitakiwa wakiwa walezi wa
mtoto Nasra, walimfanyia ukatili wa kumtelekeza na kumpa malezi akiwa
ndani ya boksi na hivyo kumsababishia magonjwa mbalimbali.
Maradhi yaliyotajwa kumkumba mtoto huyo akiwa ndani ya boksi ni utapiamlo, maumivu ya kifua na mvunjiko wa mifupa katika mwili.
Hyera alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama kutaja tarehe ya kuisikiliza.
Hata hivyo, licha ya dhamana kuwa wazi, hakuna mtu aliyejitokeza kuwadhamini washitakiwa hao hivyo kurejeshwa gerezani huku watu wakishangilia kwa kusema kwamba kitendo walichokifanya hawastahili kurejea uraiani.
Hata hivyo, licha ya dhamana kuwa wazi, hakuna mtu aliyejitokeza kuwadhamini washitakiwa hao hivyo kurejeshwa gerezani huku watu wakishangilia kwa kusema kwamba kitendo walichokifanya hawastahili kurejea uraiani.
No comments:
Post a Comment