Ghasia zaidi kupinga kombe la dunia:Polisi mmoja alijeruhiwa kwa mshale nchini Brazil
Polisi mmoja alijeruhiwa kwa mshale
Polisi
nchini Brazil wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji
katika mji mkuu Brasilia wanaopinga kuandaliwa kwa kombe la dunia nchini
humo.
Polisi
walipigwa kwa mawe huku mamia ya waandamanaji wakijaribu kufika uwanja
wa kitaifa ambako kombe litakalopokezwa washindi wa kinyang'anyiro hicho
limewekwa.
Haya ni maandamano ya hivi karibuni nchini Brazil kupinga gharama iliyotumiwa kuandaa kombe hilo.Kikundi cha watu asilia wanaodai haki zao za kumiliki ardhi walijiunga na maandamano hayo
Maafisa wakuu wanasema kuwa karibu watu 1,500 walihudhuria maandamano hayo yaliyofanyika Jumanne.
Waandamanaji
hao walijaribu kwenda katika uwanja wa kitaifa ambao utakuwa mwenyeji
wa mechi kadhaa za kombe la dunia ingawa polisi waliwazuia.
Polisi
mmoja alijeruhiwa kwa mshale uliorushwa na mmoja wa waandamanaji wakati
wa makabiliano kati ya polisi na waandamanaji hao.
Waandamanaji hao walitatiza pakubwa msongamano wa magari mjini Brasilia kwa masaa kadhaa.
Mwaka
jana takriban watu milioni moja walishiriki maandamano kote nchini humo
kutaka huduma bora zaidi za umma na kulalamikia ufisadi na gharama ya
juu iliyotumiwa kuandaa kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment