Apple kuinunua Beats
Apple kuinunua Beats kwa dola bilioni 3
Kampuni
kubwa ya teknolojia Apple imethibitisha kwamba itanunua vipokea sauti
na huduma ya kusikiliza muziki kupitia kwenye mtandao wa inteneti kutoka
kampuni ya Beats Electronics katika makubaliano ya dola bilioni 3.
Hayo yakiwa ni makubaliano makubwa katika historia ya miaka 38 ya kampuni hiyo.
Hatua hiyo inaonekana kama jitihada ya kuiendeleza sifa ya Apple katika soko la kusikiliza muziki kwenye mtandao.
Pamoja
na ununuzi huo, waanzilishi wa Beats Jimmy Lovine na msanii mtajika
katika mtindo wa kufoka na Hip Hop Dkt. Dre watajiunga na kampuni hiyo
ya kiteknolojia.
Apple kuinunua Beats kwa dola bilioni 3
Mkurugenzi
mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook alisema kuwa mkataba huo ungewezesha
kampuni hiyo ‘kuendelea kutengeneza bidhaa na huduma za muziki zenye
ubunifu duniani.’
Beats
ilianzishwa na mzalishaji wa muziki Jimmy Lovine na nyota wa mziki wa
kufokafoka, Dr. Dre, na mitambo hiyo imejulikana kuwa bora zaidi hadi
siku za hivi majuzi.
Beats ilianzisha huduma ya muziki unaolipiwa mapema mwaka huu.
Apple
ina huduma ya iTunes ambayo ndio kubwa zaidi duniani inayohusiana na
mziki, na ilianzisha kituo cha radio cha iTunes mwaka uliopita.
Apple kuinunua Beats kwa dola bilioni 3
Ijapokuwa
kampuni hiyo ya Carlifornia ndio walikuwa waanzilishi wa zamani wa
mziki wa mfumo wa dijitali, imekuwa ikikumbwa na ushindani mkubwa kutoka
kwenye huduma zinazolipiwa kama vile Spotify, Pandora na Rdio.
Hata
hivyo, huduma ya mziki ya Beats ina wateja wapatao 110,000 pekee
waliojisajili ikilinganishwa na Spotify ilio na watu milioni 10
waliojisajiliwa.
Mkataba
huo na kampuni ya Beats imeonyesha kudidimia kwa Apple ambayo
hujulikana kwa kutengeneza bidhaa mpya wala sio kununua kampuni ndogo
ndogo kama wanavyofanya wapinzani wao Google.
No comments:
Post a Comment