Sunday, 25 May 2014

AMA KWELI UZEE MWISHO CHALINZE: BABU AKAMATWA NA KABINTI GESTI



AMA KWELI UZEE MWISHO CHALINZE: BABU AKAMATWA NA KABINTI GESTI




Amakweli
dunia imekwisha! Watu wa Dar es Salaam wanasema uzee mwisho Chalinze,
Dar es Salaam kila mtu baby, kauli hiyo ilitimia usiku wa kuamkia
Jumanne iliyopita baada ya mmiliki wa Gesti ya GLP ya Mabibo Mwisho
jijini Dar es Salaam, Amos Makelle kunaswa kitandani usiku wa manane na
mfanyakazi wake aitwae Tina.






Babu Amos Makelle baada ya kunaswa akiwa kitandani  na mfanyakazi wake aitwae Tina wakiwa tayari kuchepuka.
Bosi
huyo na mfanyakazi wake walinaswa na mchumba wa Tina aitwae Salum
Mbonde ambaye alipenyezewa umbeya huyo na mteja mmoja aliyekodi chumba
kwenye gesti hiyo kwa ajili ya kufuatilia nyendo za wawili hao.
Baada ya mchumba wa Tina kupewa umbeya huo kuwa wawili hao walikuwa katika harakati za kuchepuka aliwawekea mtego.
BOSI ATOA SHINGO KUCHUNGULIA NOMA

mchumba
wa Tina wakiwa wamelizingira eneo la gesti hiyo mishale ya Saa 8:17
usiku kukiwa kumetulia tuliii... mtonyaji aliyekodi chumba kwa ajili ya
kazi maalum alimtumia ujumbe mapaparazi kuwa mzee Makelle aliyekuwa
kwenye chumba chake alitoa shingo kama mara tatu na kuangalia kulia na
kushoto kama kulikuwa na mtu aliyemuona.
Babu Amos Makelle bada ya kufumwa akiwa na mfanyakazi wake gesti.
APIGA HATUA ZA KUNYATA

Ilipotimu
saa 8:31, Mzee Makelle akiwa tumbo wazi na kipensi chake aliangalia
tena kama hakukuwa na noma, akachomoka chumbani kwake fastafasta kwa
hatua za minyato na kuzama chumba namba 104 alimokuwa Tina.
SHAAABASH... WANASWA KITANDANI

Shaaabash...
baada ya dakika chache mapaparazi na mchumba wa Tina walizama kwenye
chumba hicho na kuwakuta wawili hao wakiwa kitandani huku Tina akiwa na
nguo za ndani.
Walipohojiwa
Tina alikuwa akilia na kumuomba radhi mchumba wake na kusema bosi wake
huyo ndiye alimshawishi kuchepuka naye aliona kitendo cha kumnyima
kingesababisha apoteze ajira yake ambayo anaitegemea.
Mzee
Makelle alipohojiwa, katika hali ya kustaajabisha baada ya kujitetea
alianza kumchongea Tina kwa mchumbaake akidai si mwaminifu.
Chondechonde: Babu akiomba msamaha kutoka kwa makachero wa OFM.
“Wewe
kama huyu ni mchumba wako hilo mimi nilikuwa silijui, lakini huyu
mwanamke juzi tu kalala na mwanaume mwingine palepale gesti na kama
unabisha twendeni nikawaoneshwe kitabu cha wageni muone jina lake na la
huyo bwana,” alisema mzee huyo.
Waungwana waliokuwa wakimsikiliza mzee Makelle walimtafadhalisha kutozungumza maneno ya kichochezi na kumtaka ajitete mwenyewe.
Baada
ya sakata hilo kijana huyo alimchukua mchumba wake na kuondoka naye
ambapo paparazi ilifuatilia na kubaini kuwa bado msichana huyo
anaendelea kufanya kazi kwenye gesti hiyo.
Endapo
mfanyakazi huyo atafukuzwa kazi na bosi wake baada ya kufumaniwa
paparazi inaiomba serikali kuingilia kati ili mwanamke huyo apate haki
zake kwani bosi huyo awali alikuwa akisema huenda katika mchongo wa
kumnasa Tina anahusika.




credit:gpl


No comments:

Post a Comment