Sunday, 25 May 2014

AIBU KUBWA, MSANII JB NA STEVE NYERERE WAZICHPA JB APIGWA NGUMI TISA ZA TUMBO NA KUSHINDWA KUPUMUA KISHA AKAPIGWA TEKE LA KOLODANI NA KUDONDOKA CHINI TUKIO LATOKE BAA

AIBU
KUBWA, MSANII JB NA STEVE NYERERE WAZICHPA JB APIGWA NGUMI TISA ZA
TUMBO NA KUSHINDWA KUPUMUA KISHA AKAPIGWA TEKE LA KOLODANI NA KUDONDOKA
CHINI TUKIO LATOKE BAA




 




 Msanii Jb


 


Msanii Steve Nyerere

Katika
hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua wasanii Jakob Steven Jb na Steve
Magele Nyerere wamepiga nguvu kavukavu karibu na eneo la msiba wa
marehemu Adam Kuambiana huko Bunju huku kisa kikiwa kugeukana kwenye
dili la matangazo.




Habari
za uhakika zilizotua mezani kwa Maskanibongotz zilisema kuwa msanii
steve nyerere ndiye aliyeanza kumchokoza msanii Jb kwa kumchana baada ya
kumgeuka kwenye mchongo wa matangazo ya kampuni moja ya simu iliyopo
maeneo ya Moroco Jijini Dar.

Habari
zaidi zilisema wakati wasanii hao wakiwa baa wanakula kijala siku moja
kabla ya mazishi ya msanii mwenzao Steve alimvamia Jb na kuanza kumchana
na kumueleza jinsi alivyokuwa na roho mbaya kwa kumgeuka kwenye mchongo
wa mtangazo ya simu pale Moroco na kusema ndiyo maana anaroho mbaya.

Majibizano
hayo yalidumu kwa muda mrefu sana huku Jb akiwa kimya kwani stevu
alionekana kuumizwa na jambo hilo kwani inadaiwa zile picha za Jb kwenye
mabango ya mtandao huo wa simu mchongo alipewa na steve lakini baadae
Jb alimgeuka na kwenda kupiga mchongo kimaya kimya na kumuacha Steve
akishangaa.

Hata
hivyo Steve aliendelea kusasambua Jb mbele ya watu hali hiyo ilimfanya
Jb kunyanyuka na kuanza kufokea nae huku akimtahadharisha kama
atamfinyangafinya na ufupi wake ndipo steve nyerere aliyekuwa ameshika
chupa ya kilaji aliruka kichwa kimoja kilichompiga Jb kifuani na
kupepesuka.

Wakati
watu akijianda kwenda kuamulia basi Steve ambae aliwahi kucheza ngumi
miaka ya nyuma alimshindilia Jb ngumi kama tisa za harakaharaka sehemu
ya tumbo iliyomfanya Jb kudondoka chini na kushindwa kupumua kwa dakika
tano kisha alinyanyuka na kukalia kiti.

Tuliwasiliana na wasanii hao ili kupata ukweli wa mambo lakini kwa bahati mbaya simu zao hazikupekelewa na bado tunawatafuta.


No comments:

Post a Comment