MKE WA MTU AKAMATWA AKIFANYA UKAHABA,,,, ABAMBA AKIWA GESTI NA KONDOM KIBAO KITANDANI
Makubwa madogo yana nafuu! Kwenye kamatakamata na fumuafumua ya magenge ya biashara haramu ya ngono mjini hapa imemkumba bonge la jimama ambalo lilinaswa gesti likisubiri mteja....bonge akiwa kitandani.
Ndani ya gesti maarufu ya Itigi iliyopo maeneo ya Msamvu, inayotumiwa zaidi na madereva wa malori ya masafa marefu ndipo alipobambwa bonge ambaye katika utetezi wake alidai kuwa ni mke wa mtu.“Naombeni mnisamehe nilikuwa najitafutia riziki, baba J akijua ataniua jamani amesafiri, akirudi nimekwisha,” alisema kwa aibu mwanamke huyo. aliyejulikana kwa jina la mama J.
... bonge akiwa katika pozi la aibu baada ya kubanwa na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kitendo hicho kilikuwa cha aibu mno mbele ya jamii.Hata hivyo, pamoja na utetezi wake, bonge aliunganishwa na wenzake walionaswa kisha akapewa henyahenya na polisi kabla ya kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu kusubiri sheria kuchukua mkondo wake.
SOURCE:GPL
No comments:
Post a Comment