Wednesday, 11 December 2013

Picha Na Info, MTV Yatoa Majina Kumi Ya Wasanii Bora Wa Mwaka 2013


Picha Na Info, MTV Yatoa Majina Kumi Ya Wasanii Bora Wa Mwaka 2013

Kitua cha television MTV Kimetangaza majina kumi ya wasanii waliofanya vizuri mwaka 2013, Fahamu na hayupo na nani kafanya zaidi hapa


1. Miley Cyrus
  Huyu msanii ameweza kuteka mashabiki wa wasanii wakubwa kama Katy Perry na Lady Gaga akiwa na miaka 21 tu. Fahamu kuwa Miley amekuwa kwenye game la filamu na tamthilia kwa muda wa miaka 10 sasa ila mafanikio ya muziki yameanza kuonekana ndani ya hii miaka mitatu.   



2. Macklemore & Ryan Lewis
Kazi yao imeuza kopi milioni 6 ndani ya wiki moja tu nakama umeshawahi kuisikia nyimbo yao ya Thrift shop basi tayari unajua uwezo wa hawa jamaa. 



3. Justin Timberlake 
JT Amekuwa na mawazo mazuri kwa mwaka 2013, ameweza kufanya vizuri kwenye filamu na kuonekana bado yupo kupitia filamu ya  "Inside Llewyn Davis," ila pia kwenye muziki amefanya maajabu kwa kushika chati mara mbili kupitia matolea mawili ya album yake ya The 20/20 Experience. Pia alifanya show pamoja na NSYNC, Nakuchukua tuzo ya Moonman or Four.


4. Kanye West
Rapper, producer, fashion designer, na mwaka huu ameongeza "Christian, revolutionary, visionary products person" kwenye orodha ya mambo yake anayofanya. Kanye west ameweka mezani album ya Yeezus, amevuta jiko mtoto mzuri Kim K, Wamepata mtoto North West na Amezoa mkataba na kampuni kubwa ya Adidas. Bila kusahau album yake imeuza vizuri sana sokoni.



5. One Direction
Hili kundi halijalala mwaka huu kwani wamekuwa na show kila wiki sababu ya nyimbo bora kwenye album zao mbili zilizo fululiza kutoka. Album ya Midnight Memories imeuza kopi laki tano ndani ya wiki moja tu ikikaribia mauzo ya filamu yao ya 3-D "This Is Us,". 



6. Katy Perry
Mwaka huu amekuwa mpole kwenye skendo ila mbishi kwenye kazi, album yake mpya ya Prism ilikuwa namba moja kwenye chati mwezi wa kuni na kupata mauzo ya kopi 286,000 kwenye wiki yake ya kwanza. Nyimbo kama"Roar" na "Unconditionally" zimeshika namba moja kwenye chati ya 
Billboard Hot 100. 



7. Drake
Kanye West alitokea kwenye pati ya Drake ili tu kumpa sifa zake kwa mafanikio ya mwaka huu, rapper huyu kutoka  Toronto Canada alitoa album yake ya nne Nothing Was the Same ikiwa na collabo kubwa ya  Jay Z ila kabla ya hapo alitoa "Started From the Bottom" mwanzo wa mwaka huu ikafatiwa na "Hold on we're going home"Drizzy anatakiwa kuwepo hapa.




8. Bruno Mars 
Mwaka huu ametuendesha sana na nyimbo bora zilizoka kwenye chati kwa muda zaidi na mwezi wa nne tumeona akipokea tuzo kwa kuwa na video bora "Gorilla". Kazi zote kutoka kwenye project yake ya mwaka jana ya Unorthodox Jukebox. Fahamu kuwa jamaa ameshawahi kusema anafata nyayo za mkali mwenye heshimu kubwa duniani Frank Sinatra.


9. Lorde
Kaa mbali na huyu dada, anamiaka 17 tu ila mambo yake sio mchezo. Mwaka 2013umekuwa mwaka wake baada ya kupata mkataba na rekodi lebel kubwa Marekani ya  Universal Music akiwa na miaka 13 tu. Baada ya miaka mitatu kazi yake ya Royals ilikaa namba moja kwenye chati za Billboard Hot 100 kwa wiki zaidi ya moja.   



10. Lady Gaga
Album yake mpya inaitwa  ARTPOP na tayari wimbo wa kwanza kutoka kwenye cd hio Applause imeshika chati nchi tofauti duniani.Hivi karibuni umemskia akitengeneza pesa kubwa tu kwenye show na mauzo ya kazi mpya alizo fanya na R Kelly na  Rapper T.I



No comments:

Post a Comment